Kubainisha na kupendekeza masuala ya Mazingira yanayopaswa kuhuishwa katika mipango ya kisekta na Halmashauri kwa ujumla.
Kusimamia utekelezaji wa mikakati ya matumizi salama ya Tekinolojia ya Kisasa (Biosafety).
Kutoa ushauri kuhusu maeneo yaliyoathirika kutokana na shughuli za kiuchumi zisizo endelevu (kama vile uchimbaji wa Madini, Kilimo, Ujenzi, Ufugaji n.k).
Kuratibu miradi mbalimbali inayohusu usimamizi na Hifadhi ya Mazingira.
Kusimamia matumizi ya Rasilimali mbalimbali za Hifadhi ya Mazingira.
Kuchambua na kusambaza Takwimu za Hifadhi za Mazingira.
Kufuatilia na kushauri kuhusu utekelezaji wa mikataba na maazimio ya Kitaifa,Kikanda na Kimataifa kuhusu usimamizi na Hifadhi ya Mazingira
Kupendekeza miradi ya Hifadhi ya Mazingira.
Kupitia na kushauri kuhusu taarifa za Tathimini ya Athali za Mazingira (EIA) na mpango mkakati wa tathimini ya Mazingira(Strategic Environment Assessment)
Kupitia na kushauri kuhusu utekelezaji wa Sera, Sheria ya Mazingira na miongozo na mikakati mbalimbali kuhusu usimamizi na hifadhi ya mazingira.
Kutoa (Disseminate) Elimu ya Hifadhi ya Mazingira kwa wadau mbalimbali.
Kusimamia Usafi wa mazingira katika Halmashauri ya Mji wa Kahama
Kutoa taarifa mbalimbali za utekelezaji wa kazi za Idara kwa Mkurugenzi
Kusimamia wajibu wa haki za watumishi wote walio katika Idara ya Usafi na Mazingira