KITENGO CHA UCHAGUZI
MAJUKUMU YA KITENGO CHA UCHAGUZI
Jimbo la Kahama mjini ni Miongoni mwa majimbo mapya yaliyoanzishwa mwaka 2015 baada ya kuvunjwa kwa Jimbo la zamani la Kahama na kuzaliwa Jimbo la Kahama Mjini na Ushetu.
Kitengo cha Uchaguzi katika ngazi ya Halmashauri kinatekeleza Majukumu yafuatayo.
1.Kuratibu na kusimamia shughuli za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa na Uchaguzi Mkuu wa Rais,Wabunge na Madiwani.
2.Kusimamia na kuratibu uandikishaji wa Wapiga kura katika Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani katika Jamhuri ya Muungano.
3.Kusimamia na Kuratibu uandikishaji wa Wapiga kura katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa
(Uchaguzi wa Wenyeviti wa Vijiji,Mitaa,Vitongoji na wajumbe wa vijiji na Mitaa)
4.Kuratibu na kusimamia zoezi la ujazaji wa Rejesta ya wakazi katika Mitaa,Vijiji na Vitongoji.
5.Kupitia na Kuboresha Mipaka ya Kata,Vijiji,Mitaa na Vitongoji ili kusogeza huduma kwa Wananchi.
6.Kuendelea kutoa Elimu ya Mpiga kura kwa wananchi, taasisi za Umma na za watu Binafsi.
7.Kuendelea kukusanya takwimu za wananchi waliofikisha Umri wa Miaka 18 na kuendelea.
8.Kukusanya Takwimu za Wapiga kura waliopotelewa na Vitambulisho vya Mpiga kura na kuiarifu Tume ya Taifa ya Uchaguzi(NEC)
9.Kuandaa taarifa ya nafasi wazi za viongozi wa Serikali za Mitaa na kuomba kibali Ofisi ya Rais Tamisemi kwa ajili ya Uchaguzi Mdogo.
10.Kuratibu mafunzo ya kuwajengea uwezo kwa Wenyeviti wa Vijiji,Mitaa,Vitongoji na wajumbe wa kamati za Vijiji na Mitaa.
12.Kutekeleza Majukumu Mengine yoyote kwa Mujibu wa maelekezo toka Tume ya Taifa ya Uchaguzi(NEC)
Barabara ya Boma, Kahama
Anuani ya Posta: P.O.Box 472
Simu: +255 282710032
Simu: +255719679464
Barua pepe: md@kahamamc.go.tz / info@kahamamc.go.tz
Hakimiliki©2017. Halmashauri ya Manispaa Kahama. Haki zote zimehifadhiwa