Waziri Mkuu wa Tanzania Mhe. Kassim M. Majaliwa ameahidi ujenzi wa Kituo cha Afya kata ya Kagongwa Mjini Kahama. Ametoa ahadi hiyo Mapema leo alipokuwa akizungumza na wananchi wa Kata hiyo. Mhe. Majaliwa amesema kuwa Serikali imejipanga kusogeza huduma za afya kwa jamii.
"..Mheshimiwa Waziri baada ya kuwa wamemaliza bajeti wanaanza kupanga panga na baada ya kumaliza hii ziara akirudi Wizarani ataiingiza Kagongwa katika orodha" Amesema Mhe. Majaliwa.
Ujenzi wa Kituo cha Afya hiko kinatarajiwa kugharimu Milioni Mia tano za Ki -Tanzania.
Pia Waziri Mkuu amewaambia wananchi wa Kahama kuwa Vijiji vyote vitapitiwa na mradi wa Umeme wa REA ambao ni wa bei ya chini ambapo kila mwananchi anaweza kumudu kwani ni hitaji la Serikali kuona kuwa kila nyumba inapata huduma ya umeme.
Aidha katika upande wa Maji Mhe. Majaliwa amewahakikishia wananchi kuwa bomba linalotoka ziwa Victoria halipiti hivihivi tu ni lazima liwanufaishe wote ambao linapita.
Mhe. Waziri mkuu amewaasa watumishi wa Umma kuwa waadilifu katika matumizi ya rasilimali za Umma.
Barabara ya Boma, Kahama
Anuani ya Posta: P.O.Box 472
Simu: +255 282710032
Simu: +255719679464
Barua pepe: md@kahamamc.go.tz / info@kahamamc.go.tz
Hakimiliki©2017. Halmashauri ya Manispaa Kahama. Haki zote zimehifadhiwa