Waziri Mkuu wa Tanzania Mhe. Kassim M. Majaliwa amesema kuwa kitendo cha Halmashauri ya Mji wa Kahama kutenga maeneo makubwa ya uwekezaji na Viwanda ni jambo ambalo linapaswa kuigwa na mikoa yote ya Tanzania kwani kwa kufanya hivyo tutaenda kufanikisha adhma ya Serikali ya awamu ya tano ya kuelekea kwenye uchumi wa Viwanda.
"Nimefurahishwa sana, sana, saana na hatua iliyochukuliwa na Halmashauri ya kutenga eneo la viwanda. Ni eneo zuri ambalo lina huduma zote zikiwemo maji na umeme.. kila mfanyabiashara amepewa ardhi bure yani wewe gharama yako ni hati tu... sasa naagiza kuwa watu wote wanaofanya shughuli za mbao, kuchomelea, aluminium na kazi za aina hiyo ambao bado wapo huku mjini waende maramoja kule na ifikapo tarehe 30 mtu atakayebaki mjini Mkuu wa Mkoa nakuagiza kamata wote" Amesema Mhe. Majaliwa
Katika hatua nyingine Waziri Mkuu ameahidi kuagiza kitengo cha uwekezaji kuja kuendesha semina kiwandani hapo.
Halmashauri ya Mji Wa Kahama imetenga ekari 2500 kwa ajili ya wafanyabiashara wa mbao, aluminium na kuchomelea eneo la Zongomera.
Barabara ya Boma, Kahama
Anuani ya Posta: P.O.Box 472
Simu: +255 282710032
Simu: +255719679464
Barua pepe: md@kahamamc.go.tz / info@kahamamc.go.tz
Hakimiliki©2017. Halmashauri ya Manispaa Kahama. Haki zote zimehifadhiwa