Watumishi wa Halmashauri ya Mji Kahama waamua kuchangia ujenzi wa Madarasa. Hii imekuja baada ya kuonekana kuwa na mahitaji makubwa ya madarasa kwa mwaka huu. Haya maamuzi yamefikiwa jana Tarehe 4/01/2018 wakati wa kikao cha kujadili rasimu ya Bajeti ya Halamsahuri ya Mji wa Kahama. Mpango wa kuchangia umegawanyika katika Makundi manne ambayo ni kama yafuatayo:
1. Mkurugenzi - 100,000
2. Wakuu wa Idara na Vitengo - 50,000
3. Maafisa Ngazi ya Shahada -20,000
4. Watumishi wengine ngazi ya chini ya Shahada - 10,000
Mchango huo unaweza lipwa kwa awamu mbili yani Januari na Februari.
Akiongea dhamira hiyo, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Kahama Ndg. Anderson Msumba amesema kuwa hii ni kuwaonesha wanajamii kuwa mtoto wa mwenzio ni wa kwako, hivyo kuchangia maendeleo ya shule ni suala la kila mtu kuguswa na sio lazima uwe na mtoto anayesoma.
Aidha Msumba ametoa Rai kwa wananchi wote kujitokeza kuchangia ujenzi wa madarasa kwa namna yoyote watakavyoguswa, inaweza kuwa mchango wa Vifaa, fedha hata nguvu kazi.
Barabara ya Boma, Kahama
Anuani ya Posta: P.O.Box 472
Simu: +255 282710032
Simu: +255719679464
Barua pepe: md@kahamamc.go.tz / info@kahamamc.go.tz
Hakimiliki©2017. Halmashauri ya Manispaa Kahama. Haki zote zimehifadhiwa