Watumishi wa Halmashauri ya Mji wa Kahama leo wameadhimisha siku ya Familia duniani kwa kufanya mdahalo wa pamoja.
Katika mdahalo huo watumishi wameweza kujadiliana na kubadilishana mawazo juu ya Ukatili wa watoto, Malezi na Makuzi.
Siku ya Familia Duniani huadhimishwa kila Tarehe 15 Mei kila mwaka na nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa. Maadhimisho hayo yanatokana na tamko la Baraza la Umoja wa Mataifa 47/257 la tarehe 20 Septemba, 1993 linaloidhinisha kuwa na siku maalum kwa ajili ya familia. Tanzania ni moja ya wanachama wa Umoja wa Mataifa hivyo huungana na nchi nyingine kila mwaka kuadhimisha siku hii.
Madhumuni ya ya siku ya Familia Duniani ni kuhamasisha, himiza, kuelimisha na kutanabaisha jamii kuhusu umuhimu wa familia katika jamii kwa nia ya kuchukua hatua zinazopasa ili kuziimarisha na kuziendeleza.
Kauli mbiu ya siku ya Familia mwaka huu 2019 ni "Familia Imara kwa Maendeleo Endelevu"
Barabara ya Boma, Kahama
Anuani ya Posta: P.O.Box 472
Simu: +255 282710032
Simu: +255719679464
Barua pepe: md@kahamamc.go.tz / info@kahamamc.go.tz
Hakimiliki©2017. Halmashauri ya Manispaa Kahama. Haki zote zimehifadhiwa