Timu ya Wataalamu kutoka Manispaa ya Kahama Wametembelea Kongani ya Buzwagi (Buzwagi Special Economic Zone) na kujionea hatua iliyopo katika kuhakikisha Wawekezaji wanapatikana kuwekeza katika eneo hilo mara baada ya Mgodi kufungwa ili kuweka mwendelezo na uimara wa Uchumi wa Manispaa hiyo.
Akieleza jinsi utekelezaji wa Eneo hilo unavyoendelea Meneja Uhusiano wa Jamii na Miradi wa Buzwagi, Stanley Joseph, amesema kuwa tayari baadhi ya wawekezaji wameonyesha nia ya kuwekeza katika eneo hilo huku Baadhi yao tayari wakiwa wameshaanza uzalishaji na wengine wakiendelea na ujenzi wa Miundombinu. Ameeleza kuwa kongani ya Buzwagi ikikamilika itafanikisha kuleta fursa kubwa si kwa Wilaya ya kahama na Shinyanga pekee bali nchi nzima
Barabara ya Boma, Kahama
Anuani ya Posta: P.O.Box 472
Simu: +255 282710032
Simu: +255719679464
Barua pepe: md@kahamamc.go.tz / info@kahamamc.go.tz
Hakimiliki©2017. Halmashauri ya Manispaa Kahama. Haki zote zimehifadhiwa