Wananchi Wilayani Kahama wamehimizwa kushiriki kwenye shughuli za Maendeleo kwani jukumu la Serikali ni kumalizia pale penye jitihada za Jamii. Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Wilayani Kahama Mhe. Thomas Mnyongwa alipokuwa kwenye ziara ya Kamati ya Siasa ya Wilaya ya kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya Chama Tawala tangu 2015 hadi sasa kwenye Halmashauri ya Mji wa Kahama.
"Kamati imeridhika kwa utendaji na utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya Chama Tawala kwani tumejionea wenyewe, ila tunapaswa kujua kuwa Wananchi tumeumbwa kuwajibika, lazima viongozi tuwaambie wananchi haya mambo..wachangie ili kuwahakikishia watoto elimu bora". Amesema Mhe. Mnyongwa.
Kamati ya Siasa Wilaya ya Kahama imeanza kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya Chama Tawala kwenye Halmashauri ya Mji wa Kahama mapema leo na itahitimisha Kesho.
Miradi iliyotembelewa ni ya Sekta ya Afya na Elimu, Utawala na Viwanda. Ambapo kwa siku ya Kwanza kwenye upande wa elimu Kamati imetembelea Ujenzi unaofanywa katika Shule za sekondari Isagehe na Nyihogo, Shule za Msingi za Mayila, Bukondamoyo, Iboja na Shunu. kwa Upande wa Afya Kamati imetembelea Ujenzi wa Jengo la Wagonjwa wa nje Hospitali ya Mji wa Kahama na Kituo cha Afya Nyasubi. Kwenye Viwanda Kamati imetembea eneo la Viwanda Chapulwa na Zongomera "Dodoma". Pia kamati imetembelea ujenzi wa Jengo la Utawala linalojengwa kwenye eneo la Ofisi ya Halmashauri ya Mji wa Kahama. Baadhi ya picha za ziara hiyo hizi hapa chini:
Barabara ya Boma, Kahama
Anuani ya Posta: P.O.Box 472
Simu: +255 282710032
Simu: +255719679464
Barua pepe: md@kahamamc.go.tz / info@kahamamc.go.tz
Hakimiliki©2017. Halmashauri ya Manispaa Kahama. Haki zote zimehifadhiwa