Halmashauri ya Mji wa Kahama imeendesha mafunzo kwa wanachama na viongozi wa SACCOS mpya iliyoanzishwa na Vijana wanaofanya shughuli zao za ujasiriamali eneo la Viwanda Bukondamoyo almaarufu kama Dodoma.
Mafunzo hayo ni ya siku tatu na yameanza leo kwenye ukumbi wa Halmashauri ya Mji wa Kahama.
Mkufunzi wa Mafunzo hayo Bw. Marwa Kesanta ambaye ni Afisa Ushirika wa Halmashauri ya Mji wa Kahama amesema kuwa lengo la mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo na uelewa wanachama hao kabla hawajaanza utendaji wao.
"Halmashauri ya Mji wa Kahama inakwenda kuwawezesha Mkopo SACCOS hii na watakabidhiwa hundi ya fedha kwenye mapokezi ya Mbio za Mwenge wa uhuru na ndio itakuwa siku ya uzinduzi wa SACCOS hii, na hii ni sehemu ya matumizi ya asilimia kumi ya fedha zinazotengwa kwa ajili ya Vijana na wanawake, hivyo tunawaweka sawa waelewe mambo ya msingi ya kuzingatia" Amesema Kesanta.
Barabara ya Boma, Kahama
Anuani ya Posta: P.O.Box 472
Simu: +255 282710032
Simu: +255719679464
Barua pepe: md@kahamamc.go.tz / info@kahamamc.go.tz
Hakimiliki©2017. Halmashauri ya Manispaa Kahama. Haki zote zimehifadhiwa