Umati wa Watumishi wa Halmashauri ya Mji Kahama waliojitokeza katika makabidhiano ya Mwenge wa Uhuru kwenye kijiji cha Busenda Ushetu wameonesha 'mahaba' ya hali ya juu kwa Kiongozi wa Mbio za Mwenge na msafara wake huku wakitamani Mwenge uendelee kubaki Kahama.
Akiwakabidhi wakimbiza Mwenge Kitaifa kwa Halmashauri ya Ushetu, Mkurugenzi wa mji Kahama Ndg. Anderson Msumba ameweka wazi kuwa ingekuwa sio ratiba basi wana kahama bado walikuwa wanatamani kubaki na Mwenge wa Uhuru.
"...mimi nina kigugumizi lakini leo kigugumizi kimeongezeka kwani naambiwa nisimkabidhi Kiongozi wa mbio za Mwenge...napata tabu sana kumkabidhi lakini kwasababu ya ratibu sina budi kufanya hivyo" amesema Msumba.
Aidha Mkurugenzi amesema kuwa kikubwa kinachowafanya kutamani Kiongozi wa mbio za Mwenge na wenzake kubaki ni kwamba kuna vingi sana vya kujifunza kupitia kwao.
Mbio za Mwenge wa Uhuru umepokelewa Kahama jana tarehe 23.08.2018 na hii leo umekabidhiwa kwa Halmashauri ya Ushetu.
Barabara ya Boma, Kahama
Anuani ya Posta: P.O.Box 472
Simu: +255 282710032
Simu: +255719679464
Barua pepe: md@kahamamc.go.tz / info@kahamamc.go.tz
Hakimiliki©2017. Halmashauri ya Manispaa Kahama. Haki zote zimehifadhiwa