Diwani wa Kata ya Nyihogo Mhe. Shadrack amewataka maafisa Mifugo wa Halmashauri ya Mji Kahama kuwakamata wamiliki wa mifugo inayozurura badala ya mifugo yenyewe. Hoja hiyo imekuja kwenye kikao cha Baraza la Madiwani cha Robo ya tatu Mji wa Kahama kilichofanyika mapema leo kwenye ukumbi wa Halmashauri ya ji Kahama.
Awali alisimama Afisa Mifugo na Uvuvi wa Mji wa Kahama Ndg. Constantine Lugendo na kuelezea oparesheni inayoendelea ya kukamata mifugo yote inayozurura mjini na kwenda kuifungia Nyihogo kwenye majengo yaliyokuwa yakitumiwa na Halmashauri hiyo kisha kuwapiga faini wamiliki.
Akitoa ufafanuzi juu ya hilo Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Kahama Ndg. Anderson Msumba amesema kuwa kwa mujibu wa sheria za Miji mifugo inatakiwa kufugiwa ndani "Zero grazing" na mifugo ya Nguruwe hairuhusiwi kabisa katika makazi ya watu kwani ni kero kwa majirani kwa harufu kali ukizingatia viwanja vingi vya mjini ni "High density".
Barabara ya Boma, Kahama
Anuani ya Posta: P.O.Box 472
Simu: +255 282710032
Simu: +255719679464
Barua pepe: md@kahamamc.go.tz / info@kahamamc.go.tz
Hakimiliki©2017. Halmashauri ya Manispaa Kahama. Haki zote zimehifadhiwa