Uhitaji wa vyumba vya madarasa ni changamoto kubwa katika sekta ya elimu hivi sasa. Kwa kulitambua hilo wadau wa Elimu Mji wa Kahama wamekutana leo kujadili namna gani changamoto hiyo inaweza kutatuliwa. Baada ya mjadala mrefu wadau hao kila mmoja kwa nafasi yake alitoa ahadi ya mchango na pia maazimio 6 yameafikiwa kwa pamoja ambayo ni:
Katika taarifa iliyoandaliwa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Kahama kwa Wadau hao inaonesha kuwa Halmashauri ya Mji wa Kahama Mwaka 2017 ilikuwa na jumla ya wanafunzi 69,043 kwa madarasa ya awali hadi la saba. Kulikuwa na mahitaji ya vyumba vya madarasa 1,534, vilikuwepo 618 na upungufu 916. Idadi ya wanafunzi waliohitimu darasa la saba 2017 ni 5,391 na wanaotarajiwa kuandikishwa darasa la awali na la kwanza ni wanafunzi 25,303, Hii ni sawa na ongezeko la la wanafunzi 19,912, hivyo kufanya upungufu wa vyumba vya madarasa 1,359,Madawati 9,128 na Matundu ya vyoo 796
Pia kwa upande wa Elimu Sekondari Mwaka 2017 ilikuwa na jumla ya wanafunzi 8,721 kuanzia Kidato cha Kwanza hadi Kidato cha Sita, Kulikuwa na mahitaji ya vyumba vya madarasa 214, vilikuwepo 161 na upungufu 53. Idadi ya wanafunzi waliohitimu kidato cha Nne Mwaka 2017 ni 1,456 na wanaotarajiwa kusajiliwa Kidato cha Kwanza 2018 ni Wanafunzi 4,184, Hii ni sawa na ongezeko la la Wanafunzi 2,728 , hivyo kufanya upungufu wa vyumba vya Madarasa 102 ,Viti na meza 2,659 na matundu ya vyoo 348.
GHARAMA ZINAZOHITAJIKA KUONDOA MAPUNGUFU HAYA.
S/N
|
IDARA
|
MIUNDOMBINU HITAJIKA
|
IDADI
|
GHARAMA@
|
JUMLA
|
01
|
ELIMU MSINGI
|
MADARASA
|
1359
|
6,169,687.5
|
8,384,605,312.5
|
MADAWATI
|
9,128
|
70,000
|
638,960,000
|
||
VYOO
|
796
|
1,000,000
|
796,000,000
|
||
JUMLA
|
|
|
9,819,565,312.5
|
||
02
|
ELIMU SEKONDARI
|
MADARASA
|
102
|
6,169,687.5
|
629,308,125
|
VITI NA MEZA
|
2,659
|
70,000
|
186,130,000
|
||
VYOO
|
348
|
1,000,000
|
348,000,000
|
||
JUMLA
|
|
|
1,163,438,125
|
||
|
JUMLA YA GHARAMA YOTE |
10,983,003,438
|
Gharama za madarasa ni za ukamilishi baada ya nguvu za wananchi kujenga boma.
MIKAKATI YA HALMASHAURI
UWEZO WA HALMASHAURI
Halmashauri imetenga kiasi cha Tshs 725,073,031.60 kwenye bajeti yake ya mwaka wa Fedha 2017/2018. Na fedha hiyo itakusanywa katika vyanzo mbalimbali vya mapato ya ndani hadi mwezi Juni 2018.
MCHANGO WA JAMII
Halmashauri imehamasisha jamii kupitia vikao vya Mendeleo ya Kata kushiriki katika kuchangia ujenzi wa maboma ya vyumba vya madarasa, zoezi ambalo linaendelea mpaka sasa.
KUSHIRIKISHA WADAU MBALIMBALI WA MAENDELEO.
Halmashauri imepanga kukutana na wadau mbalimbali wa maendeleo kwa ajili ya kujadili kwa pamoja utatuzi wa mapungufu haya ili ifikapo tarehe 08/01/2018 wanafunzi wapate mahali pa kujifunzia.
Barabara ya Boma, Kahama
Anuani ya Posta: P.O.Box 472
Simu: +255 282710032
Simu: +255719679464
Barua pepe: md@kahamamc.go.tz / info@kahamamc.go.tz
Hakimiliki©2017. Halmashauri ya Manispaa Kahama. Haki zote zimehifadhiwa