Waajiriwa wapya wa Halmashauri ya Mji Kahama wamepigwa Msasa wa utendaji kazi kabla ya kukabidhiwa majukumu. Mafunzo hayo yamefunguliwa rasmi na Mkuu wa Wilaya Kahama Ndg. Fadhili Nkurlu siku ya leo katika ukumbi wa Halmashauri ya Mji Kahama.
Katika hotuba yake ya ufunguzi mkuu wa Wilaya amewasisitiza watumishi hao suala zima la kusimamia sheria na taratibu zote za serikali na kuwaomba kuwa watenda haki daima kwa kuzingatia weledi. Aidha watumishi wameaswa kuwa waadilifu katika utumishi wao na kujiepusha na vitendo vya rushwa na uvunjifu wa amani.
Mafunzo haya yamehusisha watoa mada wa kada na taasisi mbalimbali za serikali zilizopo na zinazofanya kazi Wilaya ya Kahama. Watoa mada walikuwa ni pamoja na Maafisa wa Kamati ya Ulinzi na Usalama Wilaya ya Kahama, Maafisa wa idara mbalimbali za Halamshauri ya Mji Kahama, na maafisa wa mifuko ya pensheni.
Barabara ya Boma, Kahama
Anuani ya Posta: P.O.Box 472
Simu: +255 282710032
Simu: +255719679464
Barua pepe: md@kahamamc.go.tz / info@kahamamc.go.tz
Hakimiliki©2017. Halmashauri ya Manispaa Kahama. Haki zote zimehifadhiwa