Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Kahama Ndg. Anderson Msumba mapema leo amefanya kikao na Viongozi wa Chama na Serikali wanaounda kamati ya Maendeleo ya Kata waliopo Kata ya Nyandekwa. Katika kikao hicho washiriki hao wameweza kutoa ya Moyoni kwa maslahi ya Kata yao.
"Kwa mara ya kwanza tangu niwe kiongozi wa Chama hapa katani sijawahi kuona kiongozi akija huku chini kufanya kikao kama hiki, wewe umeweza umetupa moyo sana, umeweza kutuelekeza mambo ambayo tunaahidi kwenda kuyafanyia kazi" Amesema Katibu wa Chama Cha Mapinduzi Kata ya Nyandekwa.
Kikao hiko ni matokeo ya Ziara za kikazi anazofanya Mkurugenzi wa mji wa Kahama kwenye Kata zote lengo likiwa ni kubaini changamoto na kuzitafutia suluhu.
Barabara ya Boma, Kahama
Anuani ya Posta: P.O.Box 472
Simu: +255 282710032
Simu: +255719679464
Barua pepe: md@kahamamc.go.tz / info@kahamamc.go.tz
Hakimiliki©2017. Halmashauri ya Manispaa Kahama. Haki zote zimehifadhiwa