Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera,Bunge,Kazi,Ajira na Watu wenye Ulemavu) Anthony Mavunde amewaasa vijana kufanya kazi kwa bidii na kuzitumia fursa wanazopatiwa badala ya kupoteza muda mwingi kulalamika na kutafuta pesa kwa njia za mkato.
Ameyasema hayo mapema leo akiwa kwenye Kata ya Mwendakulima iliyopo Halmashauri ya Mji wa Kahama alipokuwa akikagua eneo litakalojengwa Kitalu Nyumba (Green House). Amebainisha kuwa vijana wengi wanapenda fedha za haraka ndo maana wanajiingiza kwenye shughuli ambazo sio zenye uhakika.
Katika hatua nyingine Mhe. Mavunde ameahidi kuleta wataalamu wa SIDO na Benki ya Kilimo ili kuweza kuelimisha wananchi fursa zilizopo kwenye taasisi hizo.
Barabara ya Boma, Kahama
Anuani ya Posta: P.O.Box 472
Simu: +255 282710032
Simu: +255719679464
Barua pepe: md@kahamamc.go.tz / info@kahamamc.go.tz
Hakimiliki©2017. Halmashauri ya Manispaa Kahama. Haki zote zimehifadhiwa