Halmashauri ya Mji wa Kahama imeiwezesha SACCOS ya Vijana CDT Milioni Miamoja ili iweze kusimama na kufanya kazi. SACCOS hii inaundwa na vijana wanaofanya biashara ndogondogo maarufu kama Wamachinga ambao wametolewa mtaani na kuwekwa kwenye eneo maalum lililotengwa kwa ajili yao.
Akikabidhi hundi hiyo kwa Vijana hao Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Bi. Zainab Telack amewaasa Vijana kuitumia fursa hiyo kwa kujituma kwa uaminifu ili waweze kuyaona matunda ya SACCOS yao. Aidha Bi. Tellack amewataka vijana wengine kwenda kufanya biashara katika maeneo rsmi yaliyotengwa na kujiunga katika vikundi ili waweze kusaidiwa kujikwamua kiuchumi.
"Msingefika hapo kama mngekuwa bado mpo huko mitaani....hakuna mtu anaweza kutoa fedha kwa mtu ambaye hajulikani anakaa wapi, hajulikani anafanya nini lakini atapatikana wapi" amesema Bi. Tellack.
Katika hatua nyingine, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Kahama Ndg. Anderson D. Msumba amewaambia vijana kuwa fedha ya vijana bado zipo kikubwa ni kufuata utaratibu tu.
"Bado kuna zaidi ya Milioni miambili kwa ajili ya Vijana, jiungeni katika vikundi fuateni utaratibu kuanzia ngazi za mtaa na WDC sisi tutatoa mikopo" Amesema Msumba.
Pia ameahidi kwa vijana wote wa Kahama yeyote atakayelima Kuanzia ekari tano msimu ujao Halmashauri itamsaidia Pembejeo za kilimo yani Mbegu, Mbolea na Dawa bure.
Barabara ya Boma, Kahama
Anuani ya Posta: P.O.Box 472
Simu: +255 282710032
Simu: +255719679464
Barua pepe: md@kahamamc.go.tz / info@kahamamc.go.tz
Hakimiliki©2017. Halmashauri ya Manispaa Kahama. Haki zote zimehifadhiwa