Afisa Kilimo Halmashauri ya Mji wa Kahama Ndg. Samson Sumuni amewatoa hofu wananchi juu ya wadudu waliopo kwenye majani ya Mboga maarufu kama "Vidudu mtu" kwamba hawana madhara kwa afya ya binadamu kama inavyosambazwa kwenye mitandao ya kijamii.
Bwana Sumuni ameyasema hayo mapema leo kwenye kikao cha Baraza la madiwani cha robo ya tatu kilichofanyika katika kumbi wa Halmashauri hiyo. Amesema kuwa mdudu huyo ni Kipepeo akiwa katika hatua ya ukuaji hivyo mtumiaji wa mboga husika anapaswa kusafisha tu vizuri na kupika mboga bila kuhofia. Aidha Bw. Sumuni amewaomba wananchi kupuuzia habari zinazo sambaa katika mitandao ya kijamii kuwa mdudu huyo ni hatari na hutishia maisha ya watu.
"Hizi taarifa za kwenye mitandao ni za kupuuza tu kwani ukweli wa mambo ni kwamba yule ni Kipepeo akiwa katika hatua ya ukuaji, hivyo niwaombe watu waendelee kula mboga za majani bila hofu" Amesema Bw. Sumuni
Barabara ya Boma, Kahama
Anuani ya Posta: P.O.Box 472
Simu: +255 282710032
Simu: +255719679464
Barua pepe: md@kahamamc.go.tz / info@kahamamc.go.tz
Hakimiliki©2017. Halmashauri ya Manispaa Kahama. Haki zote zimehifadhiwa