Waziri Mkuu wa Tanzania Mhe. Kassim M. Majaliwa amesema kuwa watumishi wa Umma wanapaswa kuwajibika kwa vitendo, weledi na kwa kushirikiana. Amesema hayo mapema leo alipokuwa akizungumza na watumishi wa Halmashauri za Kahama Mji, Msalala na Ushetu katika ukumbi wa Halmashauri ya Mji wa Kahama.
"Mkuu wa idara kaa na ' subordinates' wako mtengeneze mpango kazi wa pamoja ili kila mmoja awe na uelewa wa kile kinachofanyika, tuache yale mambo ya kila kitu ufanye wewe tu, hata hizi semina unakuta unaenda wewe tu..jaribu kuwaachia na wengine waende.. uwajibikaji wa pamoja lazima utambue uwepo wa wengine" Amesema Mhe. Majaliwa.
Aidha Mhe. Majaliwa amekemea tabia ya baadhi ya watumishi kutokuwa na mahusiano mazuri katika utendaji wao wa kazi. Amewataka watumishi kuwa kitu kimoja na kufanya kazi kwa kuzingatia sheria na taratibu bila kusahau Itifaki.
Barabara ya Boma, Kahama
Anuani ya Posta: P.O.Box 472
Simu: +255 282710032
Simu: +255719679464
Barua pepe: md@kahamamc.go.tz / info@kahamamc.go.tz
Hakimiliki©2017. Halmashauri ya Manispaa Kahama. Haki zote zimehifadhiwa