Uandikishaji wananchi kwenye Orodha ya Wapiga kura kwenye Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2019 umeanza leo.
Msimamizi wa Uchaguzi wa Halmashauri ya Mji wa Kahama Ndg. Stephen Magala amesema kuwa zoezi la uandikisha ni la siku saba kuanzia leo Tarehe 8 hadi Tarehe 14 Oktoba 2019.
Katika makisio ya uandikishaji Halmashauri ya Mji wa Kahama inatarajia kuandikisha wapiga kura elfu themanini na Moja.
Aidha Bw. Magala amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi kujiandikisha ili wapate fursa ya kuwachagua viongozi wanaowataka ili kuleta maendeleo ya maeneo yao.
"Niwaombe wananchi wasichanganye uandikishaji huu na ule uliofanywa wa uboreshaji wa daftari la Kudumu la wapiga kura. Watu wote ambao wana vigezo vya kupiga kura wajitokeze kujiandikisha hata kama wameshajiandikisha kwenye daftari la kudumu la wapiga kura, uandikishaji huu unamuwezesha kumchagua kiongozi wake wa eneo analoishi, hivyo lazima wajitokeze watimize takwa lao la kikatiba" amesema Magala.
Aidha Magala amebainisha Sifa za wanaopaswa kujiandikisha ikiwa pamoja na Kuwa Raia wa Tanzania, Umri kuanzia Miaka 18 na kuendelea, Awe na akili timamu, awe mkazi wa eneo husika atakalotumia kumchagua kiongozi wake.
Barabara ya Boma, Kahama
Anuani ya Posta: P.O.Box 472
Simu: +255 282710032
Simu: +255719679464
Barua pepe: md@kahamamc.go.tz / info@kahamamc.go.tz
Hakimiliki©2017. Halmashauri ya Manispaa Kahama. Haki zote zimehifadhiwa