Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Kahama Ndg. Anderson Msumba amewataka wanakikundi waliopewa mtambo wa Kuchakata Kokoto kuwa na Subira pindi mtambo huo unapoleta changamoto kwani mbunifu wa Mtambo huo ni sehemu ya Vijana wanaojengewa uwezo na Manispaa hiyo na kupitia changamoto hizo ndipo naye anazidi kupata uelewa, uzoefu na ujuzi zaidi.
Ameyasema hayo Mapema leo alipokutana na Wanakikundi cha Wanawake cha "WACHAKALIKAJI" waliopo eneo la Lugela Mtaa wa Mtakuja Kata ya Nyahanga waliopewa Mkopo wa Mtambo huo ambao awali wamekua na malalamiko dhidi ya changamoto za mtambo huo. Katika Mkutano huo Mkurugenzi aliambatana na timu yake ya Wataalamu na wamewahakikishia wanakikundi hao kuwa muda si mrefu changamoto hizo zitakwisha kabisa.
Barabara ya Boma, Kahama
Anuani ya Posta: P.O.Box 472
Simu: +255 282710032
Simu: +255719679464
Barua pepe: md@kahamamc.go.tz / info@kahamamc.go.tz
Hakimiliki©2017. Halmashauri ya Manispaa Kahama. Haki zote zimehifadhiwa