Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Bi. Zainab Telack amesema kuwa Shinyanga imejipanga kuvunja rekodi iliyojiwekea katika Mbio za Mwenge wa Uhuru 2017 kwa kufanya maboresho na maandalizi makubwa Mbio za Mwenge wa uhuru 2018. Ameyasema hayo mapema leo wakati wa makabidhiano ya tuzo ya Mshindi wa Kwanza wa mbio za Mwenge wa Uhuru 2017 yaliyofanyika kwenye ukumbi wa Halmashauri ya Mji wa Kahama.
Akikabidhi zawadi hiyo Naibu waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Ajira na Walemavu Mhe. Anthony Mavunde amewapongeza Halmashauri ya Mji wa Kahama kwa kuwa Mshindi wa kwanza kitaifa na kuwataka kuipigania nafasi hiyo kwa mwaka huu.
"Nichukue fursa hii kuwapongeza Mkoa wa Shinyanga kwani Halmashauri zenu zimefanya vizuri katika mbio za mwenge wa Uhuru 2017, nawakabidhi zawadi hizi ziwe kama chachu katika utendaji wa kazi..." Amesema Mhe. Mavunde.
Aidha akipokea zawadi hiyo Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Kahama Mhe. Abel Shija Kishushu amemuhakikishia Naibu Waziri kuendelea kuthamini hiki walichokipata na kukifanyia kazi kwa Mbio zijazo.
Barabara ya Boma, Kahama
Anuani ya Posta: P.O.Box 472
Simu: +255 282710032
Simu: +255719679464
Barua pepe: md@kahamamc.go.tz / info@kahamamc.go.tz
Hakimiliki©2017. Halmashauri ya Manispaa Kahama. Haki zote zimehifadhiwa