Taasisi ya Utafiti wa Viuatilifu katika Ukanda wa Kitropiki (TPRI) imeendesha mafunzo kwa wakulima na wataalamu wa Kilimo wa Halmashuri ya Mji wa Kahama.
Mafunzo hayo ya Siku Moja yamefanyikia kwenye ukumbi wa Halmashauri ya Mji wa Kahama Tarehe 10/01/2019 ikiwa ni matokeo ya Ziara ya Naibu Waziri wa Kilimo Mhe. Innocent Bushungwa (Mb) aliyoifanya Mkoani Shinyanga ambapo pamoja na mambo mengine ilibainika kuwa wakulima wengi hawana elimu ya matumizi sahihi na salama ya Viuatilifu pamoja na vinyunyizi hivyo kupelekea viuatilifu kutofanya kazi inavyotarajiwa.
Mafunzo hayo yamehusisha Maafisa Ugani, Wakulima wawezeshaji, wakaguzi wa Pamba na Viongozi wa ngazi ya Wilaya na wanatakiwa kwenda kuieneza elimu hiyo kwa Wakulima wote.
Barabara ya Boma, Kahama
Anuani ya Posta: P.O.Box 472
Simu: +255 282710032
Simu: +255719679464
Barua pepe: md@kahamamc.go.tz / info@kahamamc.go.tz
Hakimiliki©2017. Halmashauri ya Manispaa Kahama. Haki zote zimehifadhiwa