Walengwa wa Mradi wa TASAF awamu ya tatu wameletewa mpango wa 'Kuweka akiba na kukuza uchumi'. Akiongea katika ufunguzi wa mafunzo kwa wawezeshaji wa TASAF, Mwezeshaji ngazi ya TAIFA amesema kuwa Mpango huu unaimarisha uwezo wa kaya wa kufanya shughuli za kuzalisha kipato ili kujikwamua kiuchumi na kutoka kwenye umaskini. Lengo kuu ni Kuwabadilisha kifikra walengwa na kuwapa stadi na uelewa wa kuzalisha kwa tija. Pia kuwawezesha walengwa kuwa na njia Zaidi ya moja ya kuzalisha kipato na kujua mbinu za kuongeza thamani ili kupata soko lililo bora
Mkakati umeandaliwa ambao umetambua maeneo makuu manne ya kutekelezwa katika mpango huu ambazo ni Kuhamasisha walengwa kuunda vikundi vya kuweka akiba Kuwapa mafunzo ya stadi mbalimbali zikiwemo za kujitambua, ujasiriamali, utunzaji wa kumbukumbu na Kuwapa mtaji wa uzalishaji, Ufuatiliaji na utoaji elimu kwa Vitendo.
Barabara ya Boma, Kahama
Anuani ya Posta: P.O.Box 472
Simu: +255 282710032
Simu: +255719679464
Barua pepe: md@kahamamc.go.tz / info@kahamamc.go.tz
Hakimiliki©2017. Halmashauri ya Manispaa Kahama. Haki zote zimehifadhiwa