Katibu Tawala Wilaya ya Kahama Ndg. Timoth Ndanya amewaasa watoto na vijana kutojishusha na kujiona wanyonge katika Maisha kwani wao wanaweza kuleta mabadiliko chanya. Ameyasema hayo leo katika maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika yaliyofanyika kwenye viwanja vya Shule ya Msingi Ilindi Mji wa Kahama ambapo alimuwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Kahama.
""Msijione nyinyi ni watoto wadogo na wanyonge hamuwezi kuleta Mabadiliko, bali mjione Mnaweza Kuleta Mabadiliko". Amesema DAS.
Aidha Bw. Ndanya amewataka wazazi na walezi wote kuhakikisha kila mtoto aliyefikia umri wa kwenda shule anaenda bila kukosa. Pia amewataka wadau mbalimbali kuendelea kusimamia haki za watoto.
Kauli mbiu ya Maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika 2018 ni "Kuelekea katika Uchumi wa Viwanda Tusimuache Mtoto"
Barabara ya Boma, Kahama
Anuani ya Posta: P.O.Box 472
Simu: +255 282710032
Simu: +255719679464
Barua pepe: md@kahamamc.go.tz / info@kahamamc.go.tz
Hakimiliki©2017. Halmashauri ya Manispaa Kahama. Haki zote zimehifadhiwa