Serikali imetangaza kuwapandisha vyeo watumishi wote wenye sifa waliokuwepo kwenye bajeti ya mwaka wa fedha 2017/18.
Hayo yamebainishwa na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Bi. Zainabu Tellack alipokuwa akiongea na wafanyakazi kwenye maadhimisho ya siku ya wafanyakazi yaliyofanyika Mjini Kahama kimkoa mapema leo.
Bi. Tellack amesema kuwa kwa muda mrefu serikali ilikuwa inapitia taarifa za watumishi na kuzihakiki ili kujiridhisha uhalali wao kwani kulikuwa na wimbi kubwa la udanganyifu.
"...tayari Serikali imeruhusu upandishwaji wa vyeo kwa watumishi wenye sifa baada ya kazi ya uhakiki kumalizika, lakini naomba niwaambie leo kwamba kazi ya upandishaji wa madaraja kwenye ngazi zote za halmashauri imeshakamilika na taarifa niliyonayo sasa ni kwamba wale wote ambao watapandishwa tayari wameingizwa kwenye mfumo ili mwezi utakaokuja waweze kupata mishahara yao mipya". Amesema Tellack.
Aidha Bi. Tellack amewaasa maafisa utumishi kutofanya kazi kwa upendeleo kwani kila mtumishi ana haki zake za msingi na watumishi wote ni sawa.
Barabara ya Boma, Kahama
Anuani ya Posta: P.O.Box 472
Simu: +255 282710032
Simu: +255719679464
Barua pepe: md@kahamamc.go.tz / info@kahamamc.go.tz
Hakimiliki©2017. Halmashauri ya Manispaa Kahama. Haki zote zimehifadhiwa