Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan amesema kuwa Serikali ina mpango wa kuweka sheria itakayomtaka kila mtanzania lazima kuwa na Bima ya Afya. Amebainisha hayo wakati akiongea kwenye Mkutano wa hadhara jana Tarehe 1/3/2019 kwenye uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Kahama.
Mhe. Samia amesema kuwa ni tamanio la Serikali kuona kwamba watu wake wanakuwa na afya njema muda wote na serikali inafanya hivyo kwasababu ugonjwa haupigi hodi.
"Bima hii kwa Familia ya watu sita inauzwa thelathini elfu tu,ukivuna na ukishakuuza mavuno yako kimbia ukachukue Bima yako kwa sababu Serikali tutakuja na sheria kwamba kila Mtanzania lazima awe na bima yake ya afya,na kuwa na bima ya afya ni kusaidia sekta ya Afya kutoa huduma kwa vizuri na kwa haraka zaidi" Amesema Mama Samia.
Barabara ya Boma, Kahama
Anuani ya Posta: P.O.Box 472
Simu: +255 282710032
Simu: +255719679464
Barua pepe: md@kahamamc.go.tz / info@kahamamc.go.tz
Hakimiliki©2017. Halmashauri ya Manispaa Kahama. Haki zote zimehifadhiwa