Serikali Mkoa wa Shinyanga imewatoa hofu wananchi waliojiunga na watakaojiunga na Bima ya Afya ya CHF Iliyoboreshwa kwa kuwahakikishia kuwa huduma za kiafya zitaboreshwa wakati wote. Hayo yamesemwa na Mkuu wa Mkoa Wa Shinyanga Bi. Zainab Tellack mapema leo alipokuwa katika ziara ya Kikazi katika kata ya Kilago Halmashauri ya Mji Kahama.
Bi. Tellack amewataka watoa huduma za afya kuhakikisha dawa zinapatikana katika vituo vyote vya kutolea huduma za afya na kutowatenga wateja wanaokuja na kadi za CHF.
Aidha Bi. Tellack amewaomba wananchi wote kujiunga na Bima ya Afya ya CHF Iliyoboreshwa kwani ni rahisi na ya uhakika.
Bima ya afya ya CHF Iliyoboreshwa inahudumia kaya ya watu sita kwa shilingi elfu kumi kwa mwaka mzima. Waandikishaji wanapatikana katika kila ofisi ya ya Kijiji/Mtaa.
Barabara ya Boma, Kahama
Anuani ya Posta: P.O.Box 472
Simu: +255 282710032
Simu: +255719679464
Barua pepe: md@kahamamc.go.tz / info@kahamamc.go.tz
Hakimiliki©2017. Halmashauri ya Manispaa Kahama. Haki zote zimehifadhiwa