Baada ya mvutano wa Muda mrefu, Shule ya Sekondari Isagehe sasa imeamuliwa isimamiwe na kuhudumiwa na Wana Kagongwa. Maamuzi hayo yametolewa na Kamati ya siasa ya Wilaya ya Kahama ilipokuwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya Chama tawala kwenye Halmashauri ya Mji wa Kahama mapema leo. Akitoa maamuzi hayo Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Kahama Mhe. Thomas Mnyongwa amewataka madiwani wa Isagehe na Kagongwa kuweka tofauti zao pembeni kuhusu suala la shule hiyo kwani wote wanaijenga Tanzania Moja.
"Kuanzia leo taarifa zote zinazo husu hii shule zitakuwa zinatolewa na uongozi wa Kata ya Kagongwa, jina litaendelea kubaki kuwa Isagehe hakuna tatizo" Amesema Mhe. Mnyongwa.
Kamati hiyo ikiwa hapo Isagehe imeweza kujionea maboma ya madarasa na mabweni yaliyojengwa kwa nguvu za Wananchi. Aidha kamati imewataka wananchi kuzidi kushiriki kuchangia ujenzi ili serikali imalizie pale watakapoishia.
Barabara ya Boma, Kahama
Anuani ya Posta: P.O.Box 472
Simu: +255 282710032
Simu: +255719679464
Barua pepe: md@kahamamc.go.tz / info@kahamamc.go.tz
Hakimiliki©2017. Halmashauri ya Manispaa Kahama. Haki zote zimehifadhiwa