Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainabu Telack ameonesha kutoridhishwa na kasi ya Suma JKT kwenye ujenzi wa jengo la Hospitali ya Mji wa Kahama. Hayo yamebainika mapema leo alipokuwa kwenye ziara yake ya kazi ya kukagua Maendeleo ya Miradi inayotekelezwa na Halmashauri ya Mji wa Kahama.
Akiwa kwenye eneo hilo la ujenzi amekuta hakuna kazi yoyote inayoendelea na alipouliza mmoja wa wasimamizi wa ujenzi huo amesema kuwa ujenzi umesimama kwa kukosekana kwa vifaa na fedha.
Aidha kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya mji wa Kahama Ndg. Anderson Msumba amesema kuwa wao kama Halmashauri wameshatoa hela kwa Suma JKT za kuendelea na ujenzi huo ila anashangazwa kuona ujenzi umesimama.
Ujenzi huo wa Jengo la Wagonjwa wa nje Hospitali ya Mji wa Kahama ulitakiwa kukamilika tangu mwezi Februari 2020 ambapo Suma JKT wakaomba kuongezewa Muda wakiahidi hadi Juni 2020 ujenzi utakuwa umekamilika kitu ambacho hakitawezekana kwani ujenzi bado umesimama.
Barabara ya Boma, Kahama
Anuani ya Posta: P.O.Box 472
Simu: +255 282710032
Simu: +255719679464
Barua pepe: md@kahamamc.go.tz / info@kahamamc.go.tz
Hakimiliki©2017. Halmashauri ya Manispaa Kahama. Haki zote zimehifadhiwa