Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga Ndg. Albert Msovela amesema utumishi wa uma unahitaji uadilifu wa hali ya juu na weledi. Ameyasema hayo Ijumaa ya Tarehe 11 Januari, 2019 alipokuwa akizungumza na kamati tendaji (CMT) ya Halmashauri ya Mji wa Kahama. Msovela amesema kuwa kila mtumishi anawajibu wa kuhakikisha mwananchi anahudumiwa kwani hilo ndilo jukumu ambalo watumishi wa Uma wamepewa.
Aidha Msovela amewataka watumishi kufanya maandalizi ya bajeti kwa kasi ila kwa ubora kwani muda sio rafiki na suala la bajeti sio la mtu mmoja. Katika hatua nyingine amesisitiza kuongeza jitihada katika kukusanya mapato, mahusiano mazuri kwa watumishi wa chini,mapambano dhidi ya Mimba za utotoni na pia watumishi kutojihusisha na masuala ya kisiasa.
Kikao hiki ni sehemu ya ziara za kikazi za Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga katika wajibu wake wa kusimamia masuala ya Utawala Bora.
Barabara ya Boma, Kahama
Anuani ya Posta: P.O.Box 472
Simu: +255 282710032
Simu: +255719679464
Barua pepe: md@kahamamc.go.tz / info@kahamamc.go.tz
Hakimiliki©2017. Halmashauri ya Manispaa Kahama. Haki zote zimehifadhiwa