Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli mapema leo amesalimiana na Wana Kahama waliojitokeza Barabarani kumlaki.
Mhe. Rais amepata fursa ya kusikiliza kero za wananchi na kuzitolea maamuzi na maagizo. Katika maagizo hayo Mhe. Rais amemtaka Mkurugenzi wa Mji wa Kahama kusitisha mpango wa Kujenga Stendi kuu ya Mabasi kwa Mkopo kwani Riba ya mikopo ya Taasisi za kifedha za kibishara ni kubwa mno, hivyo ameshauri zitumike fedha za mapato ya ndani.
Pia Mhe. Rais ameagiza ujenzi wa Shule ya Msingi Mayila ukamilike na Ifikapo Januari 2020 shule ifunguliwe. Hoja ya Shule hii imekuja baada ya Diwani wa Kata ya Nyihogo Mhe. Shadrack Mgwami kumueleza Rais kwamba kuna vifo vya watoto wa shule wanaovuka upande wa pili wa barabara kufuata shule.
Aidha katika Maelezo yake Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Kahama Ndg. Anderson Msumba amebainisha kuwa Shule hiyo ipo kwenye mpango wa Halmashauri na imetengewa Milioni miamoja kujenga madarasa nane, Vyoo na ofisi za walimu na ameahidi kufunguliwa Januari.
Barabara ya Boma, Kahama
Anuani ya Posta: P.O.Box 472
Simu: +255 282710032
Simu: +255719679464
Barua pepe: md@kahamamc.go.tz / info@kahamamc.go.tz
Hakimiliki©2017. Halmashauri ya Manispaa Kahama. Haki zote zimehifadhiwa