Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli ameamuru wale wote waliovamia na kujenga eneo la chuo cha Maendeleo ya Jamii "MWANVA" cha Mjini Kahama kuendelea kuishi katika makazi yao hayo kwani makosa yalifanywa na wataalamu na sio wao. Mhe. Rais ameyasema hayo mapema leo alipokuwa akihutubia wananchi wa Mji huu katika viwanja vya maegesho ya Malori kata ya Nyasubi.
"kwahiyo eneo hilo wale waliojenga, kuanzia leo mubaki hapohapo, zile heka arobaini zilizobaki ndizo zitakazojenga chuo, ila niwaombe wananchi wa Mwanva zile heka arobaini nimuombe Mkurugenzi azisimamie asitokee mtu azivamie" Amesema Rais.
Awali eneo hilo la Mwanva lilikuwa lina zaidi ya ekari miatatu zilizotengwa kwa ajili ya ujenzi wa Chuo cha Maendeleo ya jamii, ila baada ya kukaa muda mrefu bila kuendelezwa ndipo wananchi walivamia na kuanza ujenzi na kubakisha ekari arobaini tu ambazo katika ziara ya Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Wiliam Lukuvi aliahidi kulifanyia kazi na kupatikana kwa suluhu.
Barabara ya Boma, Kahama
Anuani ya Posta: P.O.Box 472
Simu: +255 282710032
Simu: +255719679464
Barua pepe: md@kahamamc.go.tz / info@kahamamc.go.tz
Hakimiliki©2017. Halmashauri ya Manispaa Kahama. Haki zote zimehifadhiwa