Ofisi ya Rais- Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) wakishirikiana na Mradi wa Uimarishaji Mifumo ya Sekta za Umma (PS3) wametoa Chapisho la Kiongozi cha Utaratibu wa Mafunzo elekezi ya awali kwa watumishi wapya wa sekretaieti za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa. Akiongea katika utambulisho wa Kiongozi hiko kwa wakuu wa Idara Halmashauri ya Mji Kahama, Bw. Remmy Moshi ambaye ni Mshauri wa Rasilimali watu PS3 Shinyanga, amesema kuwa Chapisho hilo limelenga kuweka utaratibu maalum wa utoaji wa mafunzo elekezi ya awali ili kuboresha utendaji kazi wa watumishi wapya na hivyo kuwa na utumishi wa Umma wenye tija, wenye kutatua changamoto na utoaji wa huduma bora kwa wananchi. Aidha Bw. Moshi ameongeza kuwa utekelezaji wa Kiongozi hiki unatarajiwa kuleta manufaa yafuatayo kwa mtumishi mpya:
Barabara ya Boma, Kahama
Anuani ya Posta: P.O.Box 472
Simu: +255 282710032
Simu: +255719679464
Barua pepe: md@kahamamc.go.tz / info@kahamamc.go.tz
Hakimiliki©2017. Halmashauri ya Manispaa Kahama. Haki zote zimehifadhiwa