Waziri wa Maji Prof. Makame Mbarawa ametoa siku 10 mradi wa maji wa Kagogwa Isagehe Halmashauri ya Mji wa Kahama kukamilika. Amesema hayo mapema leo alipotembelea maendeleo ya ujenzi wa Mradi huo wa Maji kutoka Ziwa Victoria unaopitia Isaka.
Prof. Mbarawa amesema kuwa wakandarasi wametoa ahadi nyingi kwa viongozi waliofika kwenye eneo la mradi lakini inashangaza hadi leo haujakamilika.
"Nilifikiria kumuweka ndani huyu mkandarasi japo hata siku tano ajifunze, lakini Naagiza mkandarasi afike ofisi ya Mkuu wa Wilaya leo aweke makubaliano ya kufikia Tarehe 15 mwezi huu mradi uwe umekamilika na wananchi waanze kupata maji. Kama tarehe 15 maji hayatatoka basi Mkuu wa Wilaya anajua cha kufanya" Amesema Mbarawa.
Mradi huu wa Maji una gharimu fedha za Kitanzania Bilioni ishirini na mbili na ni mkataba wa Mwaka mmoja na nusu kuanzia Juni 2017 hivyo kufikia Desemba 2018 ulitakiwa uwe umekamilika.
Waziri Mbarawa atakuwa Kahama kwa Siku mbili ambapo Kesho atakamilisha ziara yake Wilayani hapa.
Barabara ya Boma, Kahama
Anuani ya Posta: P.O.Box 472
Simu: +255 282710032
Simu: +255719679464
Barua pepe: md@kahamamc.go.tz / info@kahamamc.go.tz
Hakimiliki©2017. Halmashauri ya Manispaa Kahama. Haki zote zimehifadhiwa