Benki ya NMB Kahama imetoa vifaa vya ujenzi wa Madarasa vyenye thamani ya Milioni kumi za ki-Tanzania ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono jitihada za Serikali ya kuinua na kuboresha mazingira ya kutolea huduma ya elimu.
Vifaa hivyo vimekabidhiwa kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Kahama Ndg. Anderson Msumba mapema jana maeneo ya Shule ya Msingi Nyasubi.
Akikabidhi vifaa hivyo meneja wa benki hiyo Kanda ya Magharibi, Leon Ngowi amesema msaada huo ni mwanzo wa kutatua kero ya mbanano wa wanafunzi katika shule za msingi.
Aidha Mkurugenzi wa Mji wa Kahama amewashukuru NMB kwa kujitoa na kuwaomba kuendelea kujitoa kwani mahitaji bado ni mengi.
Akishuhudia makabidhiano hayo Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mhe. Fadhili Nkurlu ameziomba taasisi za kibenki zilizopo Wilayani humu kuendelea kuzishika mkono Halmashauri katika masuala mazima ya Maendeleo.
Barabara ya Boma, Kahama
Anuani ya Posta: P.O.Box 472
Simu: +255 282710032
Simu: +255719679464
Barua pepe: md@kahamamc.go.tz / info@kahamamc.go.tz
Hakimiliki©2017. Halmashauri ya Manispaa Kahama. Haki zote zimehifadhiwa