Halmashauri ya Mji Kahama kupitia Idara ya Mifugo na Uvuvi inatarajia kuanza zoezi la Kupiga chapa Ng'ombe wote waliopo ndani ya Mji. Afisa Mifugo na Uvuvi wa Mji wa Kahama Ndg. Constantine Lugendo amesema kuwa zoezi hilo linatokana na sheria Na 10 ya mwaka 2010 ya utambuzi, uandikishaji na utafitiliaji wa mifugo nchini, ambapo sheria hiyo inalenga kuhakikisha ufugaji unakuwa na tija kwa kuwezesha mifugo na biidhaa zake kupenya kwenye masoko ya kimataifa, kutatua changamoto ya migogoro baina ya wafugaji na watuamiaji wa ardhi pamoja na kudhibiti masuala ya wizi na kuenea kwa magonjwa ya mifugo. Wananchi wote watajulishwa namna ya uendeshaji wa zoezi hilo utakavyofanyika baada ya taratibu za awali kukamilika.
Barabara ya Boma, Kahama
Anuani ya Posta: P.O.Box 472
Simu: +255 282710032
Simu: +255719679464
Barua pepe: md@kahamamc.go.tz / info@kahamamc.go.tz
Hakimiliki©2017. Halmashauri ya Manispaa Kahama. Haki zote zimehifadhiwa