Naibu waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) , Mh. George Joseph Kakunda ameimwagia sifa Halmashauri ya Mji Kahama kwa ukuaji wa Uchumi na fursa za uwekezaji. Ametoa sifa hizo alipokuwa kwenye ziara yake ya kikazi katika Halmashauri ya Mji Kahama mapema leo Tar. 29.11.2017.
Akiwa Kahama Mh. Naibu Waziri ametembelea maeneo mbalimbali ikiwemo eneo la uwekezaji lililopo Mtaa wa Bukondamoyo maarufu kama “Dodoma” ambapo pamoja na mambo mengine amesema kuwa eneo hilo ni fursa kubwa kwa wananchi kufanya biashara na hatimaye kujikwamua katika uwekezaji.
Katika hatua nyingine Mh. Waziri ametoa wito kwa wafanyabiashara wa mbao, kuchomelea n.k ambao bado wanafanyia shughuli zao katikati ya Mji kuwa hadi kufikia Desemba 10 wote wawe wamehamia “Dodoma” na kwamba baada ya hapo msako utafanyika na hatua zaidi zitachukuliwa juu yao. “..hao ambao hawajahamia huku wanahujumu jitihada za rais za kukuza viwanda.. hatutavumilia kwa hilo” alisema Mh. Waziri.
Pia Mh. Naibu Waziri ameweza tembelea eneo ambalo ujenzi wa soko la kimataifa umesimama kata ya Busoka na kuahidi kufuatilia sababu za ukwamaji wa ujenzi. Aidha amebainisha kuwa kama soko hilo likikamilika linaweza kusaidia kuleta fursa ya kufanya biashara ki mataifa.
Maeneo mengine aliyotembelea Mh. Waziri ni pamoja na Shule ya Sekondari Nyihogo na Kituo cha afya kinachojengwa Kata ya Iyenze.
Mh. Waziri alihitimisha ziara yake kwa kuongea na watumishi wa Halmashauri ya Mji na Msalala katika Ukumbi wa Halmashauri.
Barabara ya Boma, Kahama
Anuani ya Posta: P.O.Box 472
Simu: +255 282710032
Simu: +255719679464
Barua pepe: md@kahamamc.go.tz / info@kahamamc.go.tz
Hakimiliki©2017. Halmashauri ya Manispaa Kahama. Haki zote zimehifadhiwa