Hatimaye sakata la kugombea majengo yaliyokuwa ya halmashauri ya Wilaya Kahama lililokuwa likifanywa na madiwani wa halmashauri mbili za Ushetu na mji limemalizika baada ya naibu waziri ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mh. Joseph Kakunda kuyakabidhi majengo hayo kwa Halmashauri ya Mji Kahama.
Kabla ya hapo baraza la madiwani wa halmashauri ya Ushetu chini ya mwenyekiti wake Juma Kimisha lilipinga agizo la katibu mkuu Tamisemi Musa Iyombe la kutaka majengo hayo yakabidhiwe halmashauri ya mji Kahama baada ya Ushetu kuondoka kwenda makao makuu yake huko Nyamilangano umbali wa kilometa 72 kutoka Kahama mjini.
Awali mwaka 2012 halmashauri ya wilaya ya Kahama iligawanyika mara 3 na kuzaa Ushetu, mji Kahama na Msalala huku katika mgawanyiko wa mali Ushetu ambayo kabla hajabadili jina ilikuwa ndiyo halmashauri mama iliyozaa Msalala na mji hivyo ilibaki na majengo ya ofisi zote za wilaya.
Mh. Kakunda amemuagiza Mkurugenzi wa Mji Kahama ndg. Anderson D. Msumba kuyatumia majengo hayo kwa matumizi ya ofisi na si vinginevyo ambapo Mkurugenzi wa Mji amemuahidi Waziri kuhamia majengo hayo kabla ya mwaka mpya 2018.
Barabara ya Boma, Kahama
Anuani ya Posta: P.O.Box 472
Simu: +255 282710032
Simu: +255719679464
Barua pepe: md@kahamamc.go.tz / info@kahamamc.go.tz
Hakimiliki©2017. Halmashauri ya Manispaa Kahama. Haki zote zimehifadhiwa