Mwenge wa Uhuru leo Julai 30 umekimbizwa katika Manispaa ya Kahama, ukitokea Halmashauri ya Msalala, ambapo umepitia Miradi Mitano ya Maendeleo yenye thamani ya Sh. bilioni 4.9.
Akizungumza wakati wa ukaguzi wa Miradi hiyo, Sahili amesema Miradi yote ni mizuri na na ndiyo maana ameridhia kuizindua na kuweka mawe ya msingi.
"Nimekagua Miradi yote ni mizuri Kahama mmeupiga Mwingi, endeleeni hivyo hivyo kutekeleza Miradi na kuboresha huduma kwa wananchi," amesema Geraruma.
Miradi iliyopitiwa na Mwenge wa Uhuru ni pamoja na Uzinduzi wa Mradi wa Maji katika Kata ya Ngogwa, Uwekaji wa Jiwe la Msingi kwenye jengo la uchunguzi katika Hospitali ya Manispaa ya Kahama, Uzinduzi wa Karakana ya Aluminium na Samani iliyopo eneo la Viwanda la Ummy Mwalimu Zongomera, Ukaguzi wa Kiwanda cha Kuchakata Taka ngumu kilichopo Nyasubi na Uwekaji wa Jiwe la Msingi kwenye Bweni la Wavulana wenye Mahitaji Maaalum.
Aidha nje ya Miradi ya Mwenge, Kiongozi wa Mbio za Mwenge amefanya matukio mawili ambayo ni kuzindua Jiwe la hamasa ya Anuani za Makazi kwenye jengo la Makao makuu ya Halmashauri ya Manispaa ya Kahama na Kukabidhi funguo za Magari mapya mawili ya kubebea wagonjwa "Ambulance" zilizonunuliwa na fedha za mapato ya ndani kwa Madereva.
Barabara ya Boma, Kahama
Anuani ya Posta: P.O.Box 472
Simu: +255 282710032
Simu: +255719679464
Barua pepe: md@kahamamc.go.tz / info@kahamamc.go.tz
Hakimiliki©2017. Halmashauri ya Manispaa Kahama. Haki zote zimehifadhiwa