Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Kahama Ndg. Anderson David Msumba Mapema leo amekutana na kufanya mazungumzo na Uongozi wa Shirikisho la Wamachinga Taifa pamoja na Uongozi wa Shirikisho Mkoa wa Shinyanga na Manispaa ya Kahama wakiongozwa na Mwenyekiti na Katibu.
Katika mazungumzo hayo yaliyofanyika kwenye Ofisi ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Kahama wamekubaliana kuwa na Ushirikiano wa karibu kwenye kila jambo ambalo linahusu Maslahi ya pande zote mbili.
Aidha Msumba amewataka Viongozi hao kushirikisha ofisi yake kila wanapofanya vikao vyao kwani wanategemeana na kama kuna changamoto wasisubiri vikao waende ofisini kwake kuwasilisha.
Kuanzia sasa Viongozi hao watakua wanafanya kazi kwa karibu sana na Mkuu wa Divisheni ya Biashara Viwanda na Uwekezaji katika kuhakikisha gurudumu la Maendeleo linasonga mbele
Barabara ya Boma, Kahama
Anuani ya Posta: P.O.Box 472
Simu: +255 282710032
Simu: +255719679464
Barua pepe: md@kahamamc.go.tz / info@kahamamc.go.tz
Hakimiliki©2017. Halmashauri ya Manispaa Kahama. Haki zote zimehifadhiwa