Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Bi. Zainab Tellack Leo ametembelea na kukagua ujenzi wa Kituo cha Afya katika kata ya Iyenze Halmashauri ya Mji Kahama. Akiwa katika eneo la ujenzi Mkuu wa Mkoa amesisitiza ufanisi wa ujenzi na kumtaka Mkurugenzi wa Mji Kahama kuhakikisha ujenzi unakamilika katika wakati uliopangwa.
Aidha katika maelezo ya awali kutoka kwa Mkurugenzi wa Mji Kahama kwenda kwa Mkuu wa Mkoa amebainisha kuwa ujenzi unafanywa kwa kutumia mafundi wanaopatikana maeneo husika yani "Local Fundi" na kutumia "Force Account" ambapo Halmashauri hununua mahitaji yote ya ujenzi na kazi yote husimamiwa na Mhandisi wa Halmashauri ya Mji. "Hii njia haiathiri taratibu za Manunuzi kwani yote yanayofanywa yanafuata taratibu za manunuzi na inasaidia sana kupunguza gharama kwa kiasi kikubwa" Amesema Mkurugenzi wa Mji Kahama.
Ujenzi unatarajiwa kumalizika Mwisho wa Mwezi Desemba mwaka huu, 2017.
Barabara ya Boma, Kahama
Anuani ya Posta: P.O.Box 472
Simu: +255 282710032
Simu: +255719679464
Barua pepe: md@kahamamc.go.tz / info@kahamamc.go.tz
Hakimiliki©2017. Halmashauri ya Manispaa Kahama. Haki zote zimehifadhiwa