Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan amesema kuwa utekelezaji wa ahadi zilizowekwa na Rais zinaweza kufanywa na Mkurugenzi kwani ndio mtekeleza wa ilani ya Chama Tawala kwa ngazi ya Halmashauri. Ameyasema hayo mapema leo alipokuwa akijibu hoja ya Mhe. Kibela Kishimba Mbunge Wa Kahama juu ya ahadi ya Mhe. Rais kuhusu barabara za lami kwenye Uwanja wa Halmashauri alipokuwa akihutubia wananchi.
Mhe. Samia amesema kuwa anachokifanya mkurugenzi ni sehemu ya utekelezaji wa ahadi za Rais.
"Msitegemee kwamba Rais atakuja hapa na hela aseme nimeleta hela ya kilomita kumi za barabara,hapana, naomba Halmashauri ibajeti na iweke hapo kuwa ni ahadi za rais... lakini niseme kwamba nimpongeze sana Mkurugenzi wa Halmashauri, nina taarifa kwamba amepasua barabara nyingi za vumbi, kwahiyo hiyo ndio kazi inatakiwa kufanywa.
Makamu wa Rais yupo kahama kwa ziara ya siku tatu ambayo itaishia tarehe 3/3/2019.
Barabara ya Boma, Kahama
Anuani ya Posta: P.O.Box 472
Simu: +255 282710032
Simu: +255719679464
Barua pepe: md@kahamamc.go.tz / info@kahamamc.go.tz
Hakimiliki©2017. Halmashauri ya Manispaa Kahama. Haki zote zimehifadhiwa