Mkoa wa Shinyanga umetajwa kuwa ni mmojawapo ya Mikoa yenye utoro uliokithiri kwa wanafunzi. Hayo yamebainishwa na Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru 2018 Ndg. Charles Francis Kabeho alipokuwa akitoa ujumbe wa Mwenge eneo la Kagongwa Halmashauri ya Mji wa Kahama siku ya jana tarehe 23.08.2018.
"Kwa upande wa mahudhurio ya wanafunzi Shuleni serikali imeweza kubaini kuna mikoa minne, katika mikoa hii minne kwa upande wa elimu ya Sekondari Mikoa hii inaongoza kwa utoro au ina utoro uliokithiri.. Katika mkoa wa Shinyanga na Halmashauri zake zote nyinyi mnautoro uliokithiri kwa asilimia sita pointi tatu .." Amesema Ndg. Kabeho.
Aidha Kiongozi wa mbio za mwenge amesema katika elimu ya Msingi kuna Mikoa mitano na Mkoa wa Shinyanga na Halmashauri zake hazimo kwenye orodha hiyo.
Kiongozi huyo wa Mbio za Mwenge wa Uhuru 2018 amewaasa wazazi na walezi kufuatilia maendeleo ya watoto wao Shuleni.
Barabara ya Boma, Kahama
Anuani ya Posta: P.O.Box 472
Simu: +255 282710032
Simu: +255719679464
Barua pepe: md@kahamamc.go.tz / info@kahamamc.go.tz
Hakimiliki©2017. Halmashauri ya Manispaa Kahama. Haki zote zimehifadhiwa