Halmashauri ya Mji wa Kahama imetoa Sadaka kwaajili ya Iftari na Daku kwa Waislam waliopo kwenye mfungo wa Mwezi Mtukufu.
Sadaka hiyo imetolewa Mapema leo kwenye Ofisi za Baraza la Waislam Tanzania (BAKWATA) Wilaya ya Kahama.
Akikabidhi Sadaka hiyo Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Kahama Ndg. Anderson Msumba amesema kuwa wao kama Halmashauri wameona ni vyema kwa kipindi hiki cha mfungo watoe kidogo walicho nacho kama sadaka kwa waumini waliopo kwenye mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan.
Kwa upande wake Sheikh Mkuu wa Wilaya ya Kahama Ndg. Omary Damka ameishukuru Halmashauri ya Mji wa Kahama kwa kujitoa kwa ajili ya Waislam.
Sadaka zilizotolewa kwa ajili ya Iftari na Daku ni pamoja na mchele, Tambi, ngano, Maharage,Mafuta ya kupikia na Sukari ambavyo vyote vina gharama ya fedha za Kitanzania Milioni tano.
Barabara ya Boma, Kahama
Anuani ya Posta: P.O.Box 472
Simu: +255 282710032
Simu: +255719679464
Barua pepe: md@kahamamc.go.tz / info@kahamamc.go.tz
Hakimiliki©2017. Halmashauri ya Manispaa Kahama. Haki zote zimehifadhiwa