Miradi iliyopitiwa na Mwenge wa Uhuru kwa Halmashauri ya Mji Kahama yote imekidhi vigezo na ubora wa Mbio za Mwenge wa Uhuru 2018.
Mwenge wa Uhuru kwa Halmashauri ya Mji Kahama umepokelewa leo Tarehe 23.08.2018 kata ya Kagongwa ukitokea Halmashauri ya Wilaya ya Msalala.
Mwenge ukiwa Mji wa Kahama umeweza kuzindua miradi 4 (Mradi maziwa Kagongwa, Wodi ya wazazi Isagehe, Bweni la wasichana Mwendakulima na Mradi wa maji Zongomera),
Kufungua miradi miwili (Kiwanda cha kuongeza thamani ya mazao ya kilimo Malunga na Jengo la Mama Lishe Majengo)
Kuweka jiwe la msingi mradi mmoja wa vyumba vya madarasa Mwime na Kuona mradi mmoja wa mazingira Wendele.
Miradi yote iliyopitiwa na Mwenge wa Uhuru inagharimu fedha za kitanzania Bilioni mbili nukta nne
Mwenge wa uhuru kwa Mji wa Kahama umekimbia kilomita hamsini na moja.
Kauli mbiu ya mbio za Mwenge wa uhuru 2018 ni "Elimu ni ufunguo wa Maisha, wekeza sasa kwa Maendeleo ya Taifa letu"
Barabara ya Boma, Kahama
Anuani ya Posta: P.O.Box 472
Simu: +255 282710032
Simu: +255719679464
Barua pepe: md@kahamamc.go.tz / info@kahamamc.go.tz
Hakimiliki©2017. Halmashauri ya Manispaa Kahama. Haki zote zimehifadhiwa