Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack amemaliza mgogoro wa muda mrefu wa eneo la Bonde la miwa lililokuwa linashikiliwa na mwananchi aliyekuwa anadai kuwa na haki ya kumiliki bonde hilo.
Telack alifika eneo hilo mapema jana na kukutana na Mwananchi huyo na baadhi ya wakazi wa eneo hilo lililopo Kata ya Majengo Mjini Kahama.
Katika ziara hiyo Mwananchi huyo amemuhakikishia Mkuu wa mkoa kuwa hatazuia tena shughuli zozote za uendelezaji eneo hilo na yuko tayari kutoa ushirikiano, ila ameomba kazi ya upimaji ikikamilika basi iangaliwe kama anaweza kupata eneo la kujenga.
Mgogoro wa Eneo la Bonde la Miwa umedumu kwa muda mrefu kiasi cha kuzuia hata shughuli za ujenzi wa daraja na mfereji wa kupitisha maji kukamilika kwa wakati.
Kuona mazungumzo ya Mkuu wa Mkoa akiwa eneo hilo Bonyeza HAPA
Barabara ya Boma, Kahama
Anuani ya Posta: P.O.Box 472
Simu: +255 282710032
Simu: +255719679464
Barua pepe: md@kahamamc.go.tz / info@kahamamc.go.tz
Hakimiliki©2017. Halmashauri ya Manispaa Kahama. Haki zote zimehifadhiwa