Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe. Dkt. Hussein Mwinyi leo ametembelea eneo la ujenzi wa Jengo la Wagonjwa wa nje "OPD" kwenye Hospitali ya Mji wa Kahama na kuridhishwa na Kasi ya ujenzi huo unaofanywa na Jeshi la Kujenga Taifa "Suma JKT".
Katika ziara yake hiyo Mhe. Mwinyi amesema kuwa atahakikisha vikwazo na changamoto zote zinazoonekana kuingilia ujenzi huo zinatafitiwa suluhu mapema ili kutoathiri ukamilishaji wa ujenzi huo.
Awali akitoa neno la ukaribisho Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack amemuelezea Waziri kuwa Changamoto kubwa ni ushirikiano mdogo unaotolewa na Wakala wa Majengo TBA ambao ndio Wasanifu wa Michoro inayotumika hapo ambayo imeonekana kuwa na mapungufu kadhaa na pindi wakiwasiliana nao kupata marekebisho ya Michoro hiyo wamekuwa hawafanyi kwa wakati.
Aidha kwa Upande wao Suma JKT ambao ndio Wajenzi wamemuhakikishia Waziri kuwa kama ushirikiano utakuwa mzuri wanaweza kumaliza ujenzi huo Februari, 2020 kama mkataba wao ulivyo.
Picha za Muonekano wa jengo kwa sasa:
Barabara ya Boma, Kahama
Anuani ya Posta: P.O.Box 472
Simu: +255 282710032
Simu: +255719679464
Barua pepe: md@kahamamc.go.tz / info@kahamamc.go.tz
Hakimiliki©2017. Halmashauri ya Manispaa Kahama. Haki zote zimehifadhiwa