Waziri Mkuu wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa ameongoza changizo la ujenzi wa ukuta kuzunguka shule ya Sekondari Mwendakulima Wilayani Kahama. Tukio hili limetokea mapema leo alipokabidhiwa bweni la wasichana lililojengwa na Mgodi wa Acacia Buzwagi kwenye Shule ya Sekondari Mwendakulima iliyopo Halmashauri ya Mji wa Kahama.
Katika changizo hilo Mhe. Majaliwa ametoa Mifuko ya Sementi 500 na viongozi alioongozana nao wakichangia kwa idadi mbalimbali ambapo jumla ya Mifuko ya sementi 2000 imepatikana huku Naibu Waziri Tamisemi Mhe. Joseph Kakunda akiahidi Milioni hamsini kutoka ofisi yake.
Barabara ya Boma, Kahama
Anuani ya Posta: P.O.Box 472
Simu: +255 282710032
Simu: +255719679464
Barua pepe: md@kahamamc.go.tz / info@kahamamc.go.tz
Hakimiliki©2017. Halmashauri ya Manispaa Kahama. Haki zote zimehifadhiwa