Halmashauri ya Mji wa Kahama ni Moja kati ya Halmashauri zilizopangwa kufanya kampeni ya uelimishaji na utoaji wa dawa za Magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele. Kampeni hii imelenga kundi kubwa la watoto wenye umri wa kati ya miaka 15 hadi 15.
Akiwasilisha taarifa kuhusu kampeni hii Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mji wa Kahama Dkt. Lucas Ngamtwa amebainisha kuwa magonjwa haya ni yale ambayo yanapatikana katika jamii zetu na watu wanaathirika na madhara yake husambaa. Amesema kuwa mfano wa magonjwa haya ni pamoja na Kichocho na Minyoo.
Aidha Dkt. Ngamtwa amesema kuwa madhara yatokanayo na magonjwa haya ni pamoja na:
"Magonjwa haya yanaweza kuzuirika katika jamii zetu kwa kutumia dawa za kutibu na kukinga, kuzingatia usafi wa mazingira, kutumia viatu kinga wakati wa kufanya shughuli kwenye mashamba na maeneo yenye majimaji ardhini n.k" Amesema Ngamtwa.
Utekelezaji wa zoezi hili la kitaifa linafanyika kwa kutumia fedha za wahisani kwa kupitia kitengo cha kudhibiti magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele ambao ni USAID kupitia SCI.
Barabara ya Boma, Kahama
Anuani ya Posta: P.O.Box 472
Simu: +255 282710032
Simu: +255719679464
Barua pepe: md@kahamamc.go.tz / info@kahamamc.go.tz
Hakimiliki©2017. Halmashauri ya Manispaa Kahama. Haki zote zimehifadhiwa