• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Halmashauri ya Manispaa ya Kahama
Halmashauri ya Manispaa ya Kahama

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Kahama

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mpango Mkakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Mipango, Uchumi na Takwimu
      • Maendeleo Ya Jamii
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ujenzi
      • Maji
      • Ardhi na Maliasili
      • Fedha na Biashara
      • Afya
      • Usafi na Mazingira
    • Vitengo
      • TEHAMA
      • Ukaguzi
      • Sheria
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Habari
  • Fursa za Uwekezaji
  • Huduma
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Usafi na Mazingira
    • Maendeleo ya Jamii
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Kamati ya Fedha na Utawala
      • Kamati ya Mipango Miji na Mazingira
      • Kamati ya Uchumi, Elimu na Afya
  • Miradi
    • Miradi iliyopitishwa
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi inayoendelea
  • Machapisho
    • Sheria
      • Sheria ndogo za mazingira
      • Sheria ndogo za Halmashauri
      • Tozo za Leseni za Biashara
    • Fomu
    • Miongozo
    • Fursa za Uwekezaji
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Matukio
    • Habari

Magodoro 30 yatelekezwa Kituo cha afya Mwendakulima, walioleta hawajulikani

Imewekwa: April 24th, 2018

Wananchi wa kata ya mwendakulima  halmashauri ya mji wa Kahama mkoani Shinyanga wameingiwa na hofu baada ya magodoro 30 kutelekezwa katika  kituo  cha afya  Mwendakulima huku haijulikana  aliyeyapeleka hapo.

Akizungumza leo kwenye  kikao cha baraza la madiwani wa halmashauri hiyo, Diwani wa Kata ya mwendakulima Pius Emmanuel alisema  magodoro hayo yana muda mrefu sasa tangu yapelekwe katika kituo hicho cha afya  na kwamba taarifa zinadai kuwa gari ambayo haijajulikana ni ya kampuni gani ilifika eneo hilo na kuyashusha magodoro hayo na kuondoka pasipo kusema nani amewaagiza kuyapeleka.

Emmanuel ameiomba halmashauri kwenda kuyaondoa magodoro hayo na kuyafanyia vipimo kwani yanatishia   amani kwa wananchi wa kata hiyo kutokana na kuhofu kuwa  huenda yanasumu ama madhara kwa binadamu.

Mwenyekiti wa halmashauri ya Mji wa kahama ABEL SHIJA amemwagiza Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri hiyo ANDERSON MSUMBA kuhakikisha yanaondolewa kwenye kituo hicho cha afya na kupelekwa kituo cha Polisi kwa hatua za kupata RB na kufanya upelelezi kubaini nani aliyeyapeleka katika kituo hicho.

Akijibu  kwa niaba ya Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya Mji wa Kahama,  Kaimu Mganga mkuu wa  halmashauri hiyo Dokta LUCAS DAVID amesema ofisi yake inataarifa na jambo hilo ambapo tayari wameanza mchakato wa kuyafuatilia ili kufahamu yamepelekwa na kampuni au na mtu gani katika kituo hicho cha Afya na kwamba wamekwisha litaarifu  jeshi la Polisi wilayani Kahama kwaajili ya uchunguzi zaidi.

Matangazo

  • INGIA HAPA KUPATA SALARY SLIP YAKO June 03, 2025
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI

    May 14, 2025
  • Kanuni za Maadili za Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani 2025

    April 19, 2025
  • Uboreshaji Awamu ya Pili wa Daftari la Mpiga Kura kuanza Mei Mosi

    April 16, 2025
  • Naibu Meya Manispaa ya Kahama ahimiza Ulipaji wa Ankara za Hati

    April 16, 2025
  • Angalia zote

Video

Ufafanuzi wa Mikopo ya Asilimia Kumi Manispaa ya Kahama
Video zaidi

Viunganishi vya haraka

  • Picha Mbalimbali
  • Matukio Mbalimbali
  • Kupata Salary slip
  • Mapato na Matumizi Oktoba -Desemba 2017
  • Taarifa ya Miradi ya Mwaka 2016/2017
  • Zabuni mbalimbali
  • Taarifa kwa umma

Viunganishi vinavyohusiana

  • MFUMO WA KUWASILISHA MALALAMIKO
  • Ajira Serikalini
  • NECTA
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Tovuti ya Ikulu

Wasomaji mbalimbali Duniani

world map hits counter

Idadi ya wasomaji

free HitCounter

Ramani

Wasiliana nasi

    Barabara ya Boma, Kahama

    Anuani ya Posta: P.O.Box 472

    Simu: +255 282710032

    Simu: +255719679464

    Barua pepe: md@kahamamc.go.tz / info@kahamamc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki©2017. Halmashauri ya Manispaa Kahama. Haki zote zimehifadhiwa